NGM257

Hot Newz | Fab Rayan adai kuwa yeye ndie muanzilishi wa jina la BANTU BWOY sio Big Fizzo

Spread the love

Ninaimani itakuwa sio mara yako ya  kwanza kuona au kusikia jina la Bantu Bwoy likitumika kwenye nyimbo za msanii wa muziki wa Burundi Fleva, Big Fizzo hasa katika nyimbo zake alizoziachia mwaka 2017, sasa kupitia ukurasa wake wa Facebook Big Fizzo ameandika na kudai kwamba kuna page ya facebook inatumia jina lake la bantu Bwoy.

 Tumejaribu kumtafuta muhusika wa page hiyo bila shaka tulifanikisha kumtambua ni kijana mdogo anaefahamika kwajina la Fab Rayan (facebook) uku alikubali kama yeye ndie mumiliki wa page hiyo.
Fab Rayan alidai na kusema kuwa yeye ndie mwanzilishi wa idea wa jina  la bantu bwoy na kuongeza kusema wengine wanajaribu ku kopi tu.

Kupitia maojiano na NGM257, Fab Rayan alisema ”nakumbuka nimesoma historia ya ki Bantu Primary School na hiyo idea nimeitoa kwake Juma Jux na Jules raisi wa Bitozi ila toka kitambo wananiita Bantu. Na page hiyo niliifungua Januari, 2017. Nimeanza kushangaa kusikia jina la bantu bwoy kwenye nyimbo kadhaa za jamaa fulani ata jina nasahau ila powa nimepotezea kwasababu nimeona ni jinsi gani watu wameanza kunifuatilia mpaka wasanii.”

Fab Rayan alisema kuwa anazidi kupata sms na call tofauti zikimtishia maisha endapo hatobadili jina la bantu bow na kusema:

” Ndio kuna siku nimepata call namba ambayo siijuwi baadae simu ikakata labda alikua hana vocha, nikajaribu kumpigia akajitambulisha kama yeye ni Fizzo na kuanza kunitishia maisha kisa tu ya jina la bantu Bwoy. Inanishangaza sana kuona baada ya muda anaamua kuachana na jina lake la Burundiano na kukopi jina langu, hii inanionesha kuwa mi ni mbunifu wa hali ya juu na bado atasubiri nifanye nini ili aige”. Alisema Fab Rayan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com