NGM257

Best Life Music wamwagana na Management yao ya CMG

Spread the love

Kundi la muziki kutoka Burundi Best Life Music limetangaza rasmi kuacha na management yao ambayo ilikuwa ikisimamia kazi zao za muziki upande wa usambazaji na uuzaji.

Kupitia kurasa zao za Facebook Best Life Music wameandika ujumbe mrefu ukiwafahamisha mashibiki wa muziki kwamba tayari wamemwagana na Label ya Chako Music Group kuanzia October 2 ,2018.

Best Life Music wameandika wakisema kwamba chanzo kikubwa chakuachana ni kutokana na label hiyo kutofuatisha makubaliano yao kama hawali, wamesema tena kwamba wamevumilia mengi ila sasa uvumilivu umewashinda.

Best Life Music ila wanaishukuru CMG kwakutumika nao kipindi chote hiki na wamejifunza mengi kupitia Chako Music Group.

Ikimbukwe kwamba Best Life Music na Chako Music Group wamefanya kazi nyingi kwa pamoja na kazi ya mwisho ni ngoma “DownLow” iliofanyikia nchini Uganda na kwasasa kundi hilo linafanya kazi la label ya msanii Sat B iitwayo Empire Avenue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com