NGM257

Bruno Simbavimbere (Memba), Mkuu wa Shirika la Wanamuziki Burundi afariki dunia

Spread the love

Kiongozi na Mkuu wa Shirika la Wanamuziki wa Burundi (Amical des Musiciens du Burundi) , Bruno Simbavimbere maarufu kama Memba amefariki dunia hii ijumaa 1 machi kwenye Hospital ya Mfalme Khaled (Roi Khaled) ya Kamenge.

Bruno Simbavimbere, Kiongozi wa Shirika la Wanamuziki wa Burundi

Bruno Simbavimbere amefariki baada ya kumaliza wiki nzima akiwa amelazwa kwenye hospitali hiyo, baada ya kushambuliwa na kikosi cha watu wabaya na kukatwa panga kichwani wakati akirudi nyumbani kwake Kibenga mjini Bujumbura, ijumaa ya wiki iliyopita.

Bruno alipelekwa kwenye hospitali tofauti baada ya kukatwa panga kichwani ili kupata huduma za kwanza lakini ikawa ngumu kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya zaidi.

Bruno alifanikiwa kufikishwa kwenye hospitali ya Mfalme Khaled siku hiyo ambapo alikuwa akipata matibabu mpaka kufikia hatua ya kutoeka duniani.

Kutokana na hali ya kidondo alichokipata, Bruno Simbavimbere alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa siku ya leo , lakini haikuwezekana maana Mungu alimpenda zaidi akawa amemchua uhai.

Wasanii tofauti kwenye tasnia ya muziki wa Burundi  kama T MAX, NATACHA, MT NUMBER ON, na wengine walijitolea kumsaidia ili kueneza kiasi cha pesa ambayo ilihitajika ili kukamilisha zoezi la upasuaji lakini yote yamekuwa bure maana mkono wa Mungu ulimvuta na kumrudisha alikotoka.

Bruno Simbavimbere aliwahi kuwa muandishi na mpiga ngoma mahiri sana kwenye kundi la muziki wa utamaduni (AMABANO).

Alishirikiana na wasanii wenzake wa zamani akiwemo Marehemu Christophe Matata, Alain Nova, Canjo Amisi na wengine ili kuendeleza kundi hilo.

Bruno Simbavimbere alikuwa kiogozi na mwakilishi wa Shirika la Wanamuziki wa Burundi kwa muda mrefu mpaka leo kutoeka.

Wasanii wengi wameweza kuonyesha kiasi gani habari ya kifo chake imewagusa kupitia kurasa zao tofauta za mitandao ya kijami.

Kilio kimetengwa nyumbani kwake Kibenga mjini Bujumbura ambapo alikuwa anaishi.

Tazama mahojiano ya mwisho kabla ya kifo chake , NGM TV iliyofanya na Mjomba wake Fabrice NIYERA akielezea hali yake ilivyokuwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com