NGM257

CAN 2019 : Burundi yatamba kuwatafuna Sudani Kusini nyumbani kwao Juba

Spread the love

Mbali ya kufungwa bao la kwanza katika dakika la 14 kupitia mchezaji Atak Lual, dakika ya 15 tu Burundi ilikuja juu zaidi kwa kusawazisha bao kupitia mshambuliaji wa JS Kabylie Fiston Abdul Razzk  na baada ya kumiliki mpira kuliko wenyeji, Cedric Amissi aliweza kupachika bao la pili  dakika 40.

Hata hivyo kipindi cha pili, Sudani Kusini ilijaribu kupenya na kupata bao la pili kupitia Dominic Aboi dakika la 59.

Kocha wa Burundi, Olivier Niyungeko aliweza kufanya mabadiliko ya muhimu na kumsaidia mshambuliaji wake Abdul Razzak Fiston kutamba na kuwatafuna wasudani kwa kupachika mabao matatu (76, 86, 87) na kuipelekea nchi yake kutamba ugenini kwa mabao matano kwa mbili ya Sudani Kusini (2-5).

Kwa muda huu Burundi waongoza kundi C kwa kusubiri mchezo kati Gabon na Mali, ambao wanacheza Jumamosi huko libreville.

Msimamo wa muda  : 1. Burundi, 9 pts (+6).

2. Mali, 8 pts (+4).

3. Gabon, 7 pts (+3).

4. Soudan du Sud, 0 pt (-13).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com