NGM257

Fungus Nzobikora Challenge,LION DC kutoka Kayanza waibuka mabingwa

Spread the love

FUNGUS NZOBIKORA CHALLENGE: Kundi la LION DC kutoka mkoani Kayanza wameibuka mabingwa na kupewa kitita cha laki tatu za pesa ya Burundi (300.000fbu).

LION DC kutoka Kayanza wameibuka washindi wa kwanza baada ya kuwashinda wakali kutoka DOUBLE A mkoani Bujumbura.

Ushindi wa LION DC umepatikana baada ya mashabiki wenyewe kuamua nani mshindi hapo ilikuwa baada ya majaji kushindwa kuamua wao wenyewe na kuwapa muda na nafasi kubwa mashabiki wenyewe wakaamua nani mshindi.

Ushindi wa LION DC umepamba moto baada ya kelele za mashabiki kujaa uwanja mzima.

LION DC na DOUBLE A wamepewa nafasi ya kuchuana uso kwa uso (Battle) kwa dakika moja kila kundi huku wakiucheza wimbo wa NZOBIKORA wa kwake MASTERLAND.

Baadhi ya mashabiki na watu ambao walikuwepo wameonekana kutopendezwa na ushindi wa LION DC maana walitegemea kuwa kundi la DOUBLE A ndilo lingechukua ubingwa baada ya kuonekana kufanya vizuri zaindi kwenye kiline cha uso kwa uso (Battle).Lakini nafasi hiyo imepotea ghafla baada ya kuzidiwa mashabiki na kundi la LION DC.

“Ningekuwa Jaji, DOUBLE A ndio ambao wangeibuka washindi kwa sababu wamewazidi uchangamfu kidogo LION DC kwanye kilinge cha uso kwa uso.” Amesema MASTERLAND kwenye mahojiano na NGM TV257

“Lakini naamini,asiyekubali kushindwa si mshindani, mashabiki wenyewe wameamua na kuona yupi anastahili kuwa bingwa,hivo hatuwezi kubisha.” Aliongeza Masterland.

LION DC ,mabingwa watetezi wa FUNGUS NZOBIKORA CHALLENGE wamepewa Laki tatu za burundi (300.0000 kama washindi wa kwanza, na boxi mbili zavinywaji vya FUNGUS.

DOUBLE A washindi wa pili, wameibuka na kitita cha 200.000 FBU, na boxi moja ya vinywaji vya FUNGUS.

YAMOTO DANCE nao kwa nafasi ya tatu wameipewa laki moja ya pesa za burundi (100.000FBU) na boxi moja ya vinywaji vya FUNGUS.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com