Hot news | Gaga amdiss Big Fizzo kwa video yake na kuipaisha video yake

Spread the love

Msanii wa muziki wa Buja fleva, Gaga Blue ambae anatikisa hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii na video ya wimbo wake mpya ”Mama la Mama” aliyowashirikisha wasanii wa Bongo fleva, Mr T Touch na Barakah the Prince, inadaiwa ameonesha diss ya wazi kwa video ”Konzi” ya Big Fizzo na kuipaisha video yake.

Ameonekana  mjini dar es salaam leo asubuhi akizunguukwa na waandishi wa habari wakimuhoji maswali kuhusiana na uwepo wa producer Mr T Touch kuimba kwa mara yake ya kwanza kwenye wimbo wake tofauti na jinsi wanavyo mfahamu.

Gaga Blue alisema kuwa yeye ndie aliesababisha producer huyu kuimba na ameonekana kama anaweza pande zote na kuongeza kuwa Mr T Touch anakipaji cha hali juu.

Aidha video yake imeachiwa siku moja na video  ya Big Fizzo, msanii huyu alisikika akitamka na kuweka wazi diss kwa video ya Fizzo na kusema , ” napenda sana kufanya kazi zangu hapa kwasababu  na jifunza mengi sana na kwasasa insu ya 1k viewz kwa  siku chache sio tena tatizo kwenye video zangu, nasikia  home wanashindana kwa viewz kama watoto wadogo ila tazama video yangu ya mama la mama inaiacha kwa mbali zaidi video ya Konzi ambayo tumeachia siku moja baada ya mwingine, itakuwia wepesi kubaini namna ”Mama la mama” inavyofunika ”Konzi”  kibiashara. Twende mdogomdogo”.

Alipo ulizwa kwanini analinganisha video yake na ”Konzi”  na wametaka kufahamu konzi ni video ya msanii gani kutoka Burundi, Gaga Blue alijibu na kusema, ‘huyo ni mwanamuziki  ambaye madhumuni yake ni kuimba nyimbo nzuri ili awe anasikilizwa na marafiki zake au na nduguze halafu wanaburudika, mimi sivyo”. alimalizia Gaga Blue.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat