NGM257

Hot News | Hawa ndio wasanii waliosaini mkataba na Good Father Music

Spread the love

Boss wa Studio Good Father Music, John B Pro ametangaza rasmi wasanii wanaosimamiwa na lebo hiyo huku kila msanii akisaini mkataba wa miaka miwili wa kufanya kazi na Good Father Music.

Good Father Music ni Studio ya kwanza mkoani Rumonge nchini Burundi kuanzishwa na kusimamia wasanii,  tofauti na studio zingine mkoani hapo.

Kiongozi wa Studio hiyo, John B alisema lengo la kuwakutanisha na kuwasainisha mkataba wasanii hawo ni kusaidia vijana wenye vipaji na kuifanya sana ya Burundi Fleva iendelee mbele kama nchi zingine.

Wasanii walio saini mkataba wa miaka miwili na Good father Music ni pamoja na

A-New

G-Five

Yoyo Classic

El-Alfred (gospel)

Bila sha hawa tuliowataja hapa juu ndio wasanii watakaosimamiwa na Good father Music ya John B Pro ambayo kazi yake ni kutangaza kazi zao zote wanazofanya huku kubwa likiwa ni kuwasaidia wasanii hawo kuonesha vipaji vyao kwa faida ya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com