NGM257

Hot News | King Touch kufanya wimbo mkubwa na Kingorongoro?

Spread the love

Mwanamuziki wa Buja Fleva anaefanya vizuri na wimbo wake ”Sikujuwa”, King Touch ameiambia NGM257 kuwa mazungumzo kwaajili ya kufanyika wimbo na rapa anaejihita SIMBA mwenye ROHO ya PAKA, Magic Soldier Kingorongoro yapo sehemu  nzuri.
King Touch ni mmoja kati ya wasanii ambao Kingorongoro anawaadmire sana na King Touch ni mmoja kati ya mashabiki wake ndio moja ya sababu wawiwili hawa kushirikiana.
Kingorongoro alisikika nakufunguka kuhusu collabo yake na King Touch na kusema kuwa anapenda msanii anaebadilika ambae habaki pale pale na kumtaja King Touch  kama ni mtu ambaye anafunguka zaidi kwenye suala la muziki.

Aidha, King Touch amedai kuwa anataka kufanya wimbo mkubwa na Kingorongoro itakayo beba jina la WANATEMA TAARAB.
” mazungumzo kati yangu na Simba mwenye Roho ya Paka (Kingorongoro) kwaajili ya kufanya wimbo huo yapo sehemu nzuri sana na ninaimani itakuja kuleta mabadiliko kwenye muziki wa kizazi kipya because ni wakali wawili wamekutana. Mimi na Kingorongoro hatutakiwi kufanya kazi nyepesi, tunatakiwa kufanya wimbo mkubwa, wimbo wenye uzito ili tujenge kazi yenye ubora, kazi yenye kumbukumbu pia wimbo ambayo itaishi, itaingiza pesa na itatutoa kutoka hatua hii kutupeleka hatua nyingine.” Alisema King Touch.
KWAHIYO WAPENZI WAMUZIKI TUSUBIRIE KAZI NZURI KUTOKA KWA WAKALI WAKO WAWILI KING TOUCH PAMOJA NA KINGORONGORO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com