NGM257

Hot News| KIRIKOU tayari kuvunja ukimya na maneno ya watu.

Spread the love

Baada ya muda mrefu akiwa kwenye ukimya ambao ulimpelekea mpaka kuanza kuzungumziwa kivingine na watu huku wengi wakijiuliza nini kilichomfanya mpaka kuingia chini ya uongozi wa Kampuni ya BANTU BWOY inayomilikiwa na Mwanamuziki BIG FIZZO kwa sababu kulikuwa hakuna hata fununu za kijana huyo kuachia kazi yoyote.

Ukimya wake kumbe haukuwa wa kawaida.Tulijaribu kumtafuta BIG FIZZO atwambie nini kinaendelea kwa KIRIKOU.Alitwambia kuwa kijana tayari anakaribia kuachia wimbo wake wa kanza .Aliongezea na kutwambia kuwa kijana huyo ashaRekodi nyimbo nyingi kwa hiyo mashabiki wake wakae mkao wa kula maana wimbi la nyimbo lazima liwakumbe.

Kwenye zile picha ambazo zinaonekana kila kona ni moja kati ya picha ambayo inamuonyesha kijana huyo (KIRIKOU) akiwa amesimama kwenye jiwe huku akiwa ameshikiria bendera kwa juu huku akiwa na watoto wengine kitu ambacho mpaka sasa kinawapa hofu mashabiki na wapenzi wa muziki mzima wa BUJA FLEVA nini kitakuwa kwenye wimbo wake wa kwanza?

Baki na sisi kwa kila habari.Utazipata kadri zitakavyopatikana.

Sikiliza wimbo wake wa mwisho ambao alifanya na MASTERLAND kabla ya kuingia BANTU BWOY

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com