NGM257

Hot News | T Max asema haya kuhusu muziki wa Buja Fleva na kazi zake

Spread the love

Ikiwa umekua ukijiuliza kuhusu muziki wa Burundi kipi kifanyike ili uendelee mbele kama nchi zingine, basi rapa T Max amejibu swali lako. Mwana hip hop huyu amefunguka na kusema nyimbo za  Burundi hazifiki popote ni kutokana na ukosefu wa Bidii na uwekezaji za wasanii wa Burundi.

T Max alisema muziki unahitaji mambo mengi sana na kuwataka wasanii wa burundi kujiuliza swali je wewe unataka kuwepo kwenye kundi gani? na kuongeza  lazima uamue leo kukataa kuwa chini, tena usikubali kuishia daraja la wastani pia pambana kufika juu kabisa ya kilele.
T Max alisema kuwa muziki unahitaji maarifa, akili ya kiubunifu, utundu, ujanja, uwezo, kipaji, uvumilivu na bahati.

Rapa huyu ambae anatarajia kuachia video yake mpya akimshirikisha rapa maarufu Ney wa Mitego wa Bongo fleva, alifunguka kuhusu umuhimu wa kufanya kazi na wasanii  , ma producer na ma director maarufu duniani.

” Muziki sio kazi ya lelemama, muziki kama pesa unahitaji maarifa ya kibiashara, uvivu ni aduwi wa wanamuziki wengi hapa nchini kwetu, kunasehemu unaweza ukafika wanakuuliza kazi zako, umefanya  katika studio gani na producer au director gani, kufanya kazi na watu maarufu ni  kuipa nguvu kazi zako tofauti na kufanya kazi na wasio maarufu, kwasasa muziki umebadilika, rap ya sasa ni tofauti na ile ya zamani kwasasa na rap tofauti na wakati ule. ninaimani watu wengi wanasubiri kazi zangu kwa hamu na bila shaka nina mengi mazuri tu mwaka huu lazma tufanye tofauti ili muziki wetu ufike mahali pazuri”.

Aidha, kwa sura hii utagundua ni kwanini wasanii wengi wana sauti nzuri na vipaji lakini hawajawahi kuwa nembo sokoni, nyimbo nzuri ni nyingi Burundi lakini hazitengenezi pesa kulingana na uhalisia wa thamani yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com