HOT NEWS| TOFY GAS ameahidi kutoa zawadi kabla ya kurudi SOUTH AFRICA.

Spread the love

Kwa muda mrefu akiwa anaendeleza kazi zake za muziki ambazo zilizokuwa zimemleta Nchini Burundi,Mwanamuziki TOFY GAS ameahidi kuacha zawadi kabla ya kurudi alikotokea Nchini afrika kusini (SOUTH AFRICA).

Akizungumza na waandishi wa habari wa NGM257 amesema kuwa kabla ya kuondoka ataachia wimbo wake mpya mwingine ambao alihakikisha kuwa utabeba jina la SANOLA japo hajapenda kufunguka na kuelezea nini ambacho kitakuwemo ndani ya huyo wimbo.

Alipoulizwa nini ameona kama mabadiriko kwenye muziki wake kuanzia alipofika.Amesema kuwa amejifunza mengi kutokana na jinsi gani watu wengi hawaelewi umuhimu wa vipaji vipya.

TOFY GAS tangu afike Nchini Burundi alikamilisha nyimbo mbili za kushirikiana.Moja NATAMANI aliyomshirikisha  FABILOVE,Pili:TOUCH aliyomshirikisha MAGIC SOLDIER (KINGORONGORO).

Nikukumbushe kuwa TOFY GAS ndie mwanamuziki wa kipekee aliyetokea kuwa kivutio kikubwa kwa Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, TID na kufanya nae nyimbo mbili.KWANINI MIMI na WOMAN ya TID aliyomshirikisha TOFY GAS mwenyewe baada ya kuvutiwa na uimbaji mzuri wake.

TOFY GAS anajiandalia kurudi nyuma alikotokea SOUTH AFRICA.Kwa mjibu wake amesema kuwa kuna kazi nyingi za muziki ambazo inatakiwa azifanyie huko huko kwa sababu ya mahitaji fulani ambayo anaona kuyapata hapa Burundi inaweza kuwa vigumu.Hatajajua ataondoka siku gani ila alichotuahidi ni kwamba atawaaga mashabiki wake na wapenzi wote wa muziki wa Burundi kwa ujmla.

Endelea kuburudika na wimbo wake KWANINI MIMI aliomshirikisha TID kutoka Tanzania.

SHARE NA WENGINE HABARI HII.

Related Post

You May Also Like

One thought on “HOT NEWS| TOFY GAS ameahidi kutoa zawadi kabla ya kurudi SOUTH AFRICA.

  1. I have checked your page and i have found some duplicate content, that’s why you don’t
    rank high in google’s search results, but there is a tool that
    can help you to create 100% unique articles, search for: SSundee advices unlimited content for your
    blog

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat