NGM257

Hot Newz| TOFY GAS kufanya kazi kubwa SOUTH AFRICA.

Spread the love

 

Baada ya muda mrefu akiwa hapa Nchini Burundi,Mwanamuziki wa kizazi kipya TOFY GAS tayari hapatikani tena Nchini BURUNDI.Kwa mjibu wake mwenyewe anasema kuwa tayari ashatua SOUTH AFRICA ambapo anafanyia kazi zake za kila siku.

TOFY GAS ameondoka akiwa amekamilisha nyimbo kali ambazo zimeweza kumjengea jina lake na kuupanua muziki wake kwa ujumla kama NATAMANI akiwa na FABELOVE,TOUCH akiwa na MAGIC SOLDIER KINGORONGORO pamoja na SANOLA akiwa pekee yake.

TOFY GAS akiongea na mwandishi wa NGM amesema kuwa amejipanga kufanya mambo makubwa kwa sababu SOUTH AFRICA ni kama nyumbani.

Ameongeza akisema kuwa huenda hata VIDEO ya SANOLA akaifanyia hapo hapo.

Endelea kuitazama video yake ya KWANINI akiwa na TID.

Usisahau kushare habari hii na wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com