NGM257

Kipaji cha Magic Kingorongoro chazidi kuwashangaza wengi (BONGO) Tanzania.

Spread the love

Magic Soldier Kingorongoro moja ya rapa ambae anazidi kuwaaminisha wadau wa muziki Burundi kwamba Hip Hop inauwezo mkubwa wa kuvuka boda kama wanavyofanya wa bana puwa.

Baada ya kujiunga na label ya TNB(Trust No Body) inayomilikiwa na Wanda Boy nchini South Africa, Magic Soldier amezidi kupiga hatuwa moja maridadi ni baada tu ya kujielekeza nchini Tanzania.

Kwasasa staa huyo tayari amezikamilisha collabo na mastaa wa muziki nchini Tanzania akiwemo Country Boy ,Barakah Da Prince,… na wengine ambao wanazidi kumpa shavu kwenye ngoma zao kutokana na kipaji chake kilichojaa ubunifu na floo za kutekenya sikio la msikilizaji.

Akiongea na NGM257 ,Magic amesema : “Tayari nimezikamilisha ngoma zangu nahivi tupo tunazikamilisha video za ngoma izo na director wa video nitawajuza jina lake hivi karibuni.”

Magic aliongeza :”Ngoma zote zipo chini ya Producer Yogo wa Spice Music Dar es salaam,na nina collabo ambazo nimewashirikisha wasani wa hapa bongo na zingine ambazo nimeshirikishwa na wasani wenzangu wa Tz ambao waligunduwa kipaji changu,pia nina ngoma zingine ambazo nimefanya kama solo artiste.
Na kuhusu kuachia kazi hizo,iyo ni kazi ya management ndio wataamua chakufanya,nawaomba mashabiki zangu na mashabiki wa muziki mzuri wakae wakula maana muda wa kazi baada ya kazi umewadia”;aliongea Kingorongoro.

Ikumbukwe kwamba huyu ndie rappa Burundi ambae tayari ameshazifanya collabo nyingi na mastaa wa muziki wa kizazi kipya nchini Burundi ambao ni Big Fizzo,Sat-B,Lolilo na wengine wengi na kwasasa Magic anazidi kufanya vizuri na kibao chake “Vunja Goti” alichoshirikiana na Producer Kolly The Magic.

Endelea kufuatilia tovuti zetu za www.ngm257.com zitakujuza mengi kuhusu mkali huyo wa miondoko ya Hip Hop.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com