NGM257

Kuna wasani wataishia kumaliza viatu kama hawatokuwa na jicho la tatu kama Natacha na Vichou Peace & Love.

Wasani wetu funguweni macho mjuwe chakufanya ili mpate pesa.

Wasanii wengi wa Burundi kwa sasa wengi wao hali zao ni mbaya kifedha na hii ni kutokana na ukweli kwamba zile system za zamani za kusubiria promota aje akulipe laki tano ili uende ukafanye shoo sehemu zishaanza kufa kutokana na hasara kubwa wanazopata.
Hiki ndio kinawafanya wasanii wengi wanateseka na njaa mtaani mana wamekosa akili za kujiongeza na kuangalia wanaweza tumia fursa gani ambazo zitawapa kipato.

Hebu leo angalia wasanii hawa Natacha na Band ya Peace & Love inayoongozwa na Vichou Nzigamasabo wanazidi kuizunguka mikoa yote ya Burundi ili wakuze majina yao na wapate kipato bila kutegemea sapoti ya kipesa ao kupelekwa na mtu yeyote uko.
Kinachofanya wapokelewe uko kama watu wakubwa kwenye muziki ni kwasababu wali base zaidi kwenye nyimbo za kuwafundisha raia kuipenda nchi yao na kudumisha amani kwenye nchi bila kusahau haki za kibinadamu na kutetea haki za kina mama.

Na title za nyimbo hizo ndizo wanazotumia kwenye Concert zao kama jina la Tour .
(Mfano : Natacha “Uburundi Bwacu Tour”).

Hapa ni somo kwamba kuna muda inabidi wasanii waanze kutunga nyimbo kwa target za kuhakikisha nyimbo husika inaweza kumpa hata title ya shoo angalau ikampatia vihela vya kujikimu.

Naamini kwa sasa Natacha na Vichou Peace & Love wana nafasi kubwa ya kupata hela kupitia matumbuizo mbalimbali ila kutokana na brand zao kuwa kubwa wanaweza kataa kufanya matumbuizo hayo kwakua labda watakuwa na target zingine kwenye muziki wao, ila naamini kuna wasanii wengi ambao wangekuwa na jicho la tatu juu ya hili wangekuwa wanatengeneza fedha sana.

Lakini leo wasanii wamekaa hawataki hata kuchanganua akili zao na kuangalia fursa zinapatikana wapi.

Baririmvyi bacu kanguke mwiyumvire ico mwokora kugira mwiteze imbere mwongere muteze imbere umuziki wanyu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com