NGM257

L.K.Z Da Classic amjibu Kingorongoro na kumpongeza Natacha

Spread the love

Msanii çhipukizi wa Buja Fleva, L.K.Z maarufu Da Classic baada ya kutambulishwa kama msanii aliyekuwa chini ya management ya Jay Fire ambae alitangaza kuachana na muziki na kumuandaa kijana huyu ili achukue nafasi yake, amjibu rapa Magic Soldier maarufu Kingorongoro kwa kauli yake aliyoitamkah mbele ya waandishi wa habari kwa kusema kwamba “wasanii wa Burundi wana kipaji cha kuimba Live kuliko wa Bongo ila tatizo ni kujiendeleza

Da Classic alisema, “Kingorongoro ni msanii mkubwa ana kipaji cha kuitangaza Buja Fleva mbali zaidi ila kwa kauli hiyo naona hajachukua nafasi ya kutambuwa kuwa Kila chenye faida kwa namna moja huwa na hasara kwa namna nyingine. Kuna wasanii kwasasa wanajiendeleza na wanaonesha juhudi zao ila tatizo inakuja haujatambuwa kwasasa kama muziki ni kuwekeza kiasi kikubwa na duniani kote, muziki wa kisasa unabebwa sana na video nzuri. Yaani hata kama msanii akiwa mahiri namna gani kwenye uimbaji, kama nyimbo zake hazina video zilizotengenezwa kwa ubunifu zenye kuvutia basi bora aache muziki.

Aidha, Da Classic alichukua fursa ya kumpongeza mwana muziki wa Kike, Natacha kwa video yake mpya aliyoiachia hivi karibuni akimshirikisha Fally Ipupa wa DR Congo na kusema

kwasasa tumpongeze mwana mama Natacha sana na tutaendelea kujivunia uwepo wake kwasasa anawekeza sana na bila shaka tutatoboa kupitia Natacha, kumbe huyo kingorongoro atambuwe kama Burundi tunajiendeleza ila ukame wa vituo za radio na TV zinazo sikika nje ndizo hatuna.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com