NGM257

Life style| Yafaham magonjwa sita ya u-ume

Spread the love

Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa au matatizo anayoweza kumtokea mwanaume katika uume wake kwa namna mbali mbali.

Tutayataja kwa ufupi :

1. PRIAPISM.

Ni hali ya kusimama kwa uume moja kwa moja zaidi ya saa 4 .

2. PEYRONIE’S

Ni tatizo la uvimbe katika tishu ya uume na kusababisha uume kupinda na kuwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

3. BALANITIS.

Ni Maambukizi katika kichwa cha uume.

Tatizo Namba mbili hapo juu ndio upindaji usio wa kawaida wa uume na tatizo hili linaweza kumtokea mtu kama amepata ajali Au wakati wa kufanya tendo la ndoa.

4. PHIMOSIS.

Ni tatizo la kukaza au kubana kwa ngozi ya uume (foreskin) -govi na kutoweza kuirudisha nyuma.
Tatizo hili hutokea zaidi kwa watoto au watu wazima ambayo hawajatahiriwa.

5. PARAPHIMOSIS.

Tatizo hili ni kama la hapo juu ila hapa ngozi ya govi inakuwa imejikunja juu ya kichwa cha uume na kushindwa kurudi katika hali yake ya kawaida.
Nalo pia huwatokea zaidi wasio tahiriwa na watoto.

6. SARATANI YA UUME.

Ijapokuwa sio tatizo linatokea sana kwa wanaume
Ni tatizo linaanzia kwa seli za ngozi za uume kubadilika.

NI WAKATI GANI UMUONE DAKTARI?

Ukiwa na mojawapo Kati ya haya ni vyema kumuona Daktari aliyekaribu nawe kwa uchunguzi zaidi.

1. Maumivu katika uume
2. Kuwa na uvimbe katika uume au uume kuvimba.
3. Kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida katika uume.
4. Kuwa na vipele visivyopona au vidonda katika uume
5. Kutokwa na kibonge cha damu wakati wa kwenda haja ndogo au kwenye shahawa.
6. Unasimamisha kwa muda mrefu zaidi saa 4 na uume kushindwa kurudi katika hali yake ya kawaida

7. Ngozi ya govi kukaza na mkojo kutotoka vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com