NGM257

Lifestyle:STAAJABIKA NA RAIS MASKINI KULIKO WOTE ULIMWENGUNI,RAIS WA URUGUAY.

Spread the love

Ni kawaida kukuta maisha wanayoishi wanasiasa ni tofauti na wapiga kura wao ,lakini sio hivyo kwa Rais wa Uruguay ambae anaishi kwenye maeneo ya mashambani na anatoa sehemu kubwa ya kipato chake kusaidia watu masikini.

Jina lake anaitwa Jose Alberto Mujica Cordano alizaliwa mwaka 1936,May 20.Ila kwa sasa ameshastaafu urais.

1. Yani nguo zake zinafuliwa kawaida na kuanikwa nje tu,pia maji anayotumia ni ya kisima.

2. Analindwa na Polisi wawili na mbwa na alikataa kukaa kwenye nyumba ya serikali aliyopewa na badala yake akaenda kuishi kwenye nyumba ya mke wake huko mashambani ambako kuna mazingira ya kimasikini sana ikiwemo barabara mbovu nje kidogo ya mji wa Montevideo .

3. Rais na mkewe hufanya kazi ya kuotesha maua wao wenyewe yakiwa ni maisha ya kipekee kusikia ni ya Rais wa nchi.

4. Mujica anatoa asilimia 90% ya mshahara wake wa kila mwezi kusaidia watu masikini huku akisema :”Naweza nikaonekana kama Mzee wa jadi lakini maisha haya nimeyachagua mwenyewe,naweza kuishi vizuri na kile nilichonacho.

5. Gari anayotumia ya mwaka 1987 aina ya Volkswagen Beetle ( mgongo wa chura).

6. Mujica aliwahi kupigwa risasi mara sita na alitumikia kifungo miaka 14 jela ambapo muda wake mwingi alikuwa katika mazingira magumu na kutengwa ,mpaka alipoachiliwa huru mwaka 1985 wakati Uruguay ilivyorudi kwenye demokrasia.

7. Akiwa jela Mujica anasema hali ile ilimbadilisha mtazamo wake juu ya maisha na anakwambia :” Mimi naitwa Rais masikini lakini mimi sihisi umasikini wowote,watu masikini ni wale ambao kazi yao ni kuishi maisha ya gharama ambayo inawasababisha kufanya kazi sanaa ili waendelee na maisha ya gharama na kupata zaidi.”

Kwa stori na habari nzuri za kijanja endelea kufuatilia tovuti zetu www.ngm257.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com