NGM257

Linah Blanche aingia kwenye muziki na miguu yote miwili na “I Don’t Care” .

Spread the love

Baada ya kufanya hit nyingi akiwa na mpenzi wake Vivi Muyomba kwenye “SIKILIZA BAND“, Linah Blanche amethibitisha kuingia mzima mzima katika muziki kama msanii wa kujitegemea (Solo Artist).

Msanii huyo wa kike mkali wa masauti ameyambia NGM257 kwamba Sasa hivi anataka afocuse na career yake kama solo artist na hivi karibuni ataachia ngoma mpya “I don’t care” (Sijali).

Ngoma hiyo itakuwa ya kwanza kufanya kama solo artist baada ya kuacha kufanya kazi pamoja na Vivi Muyomba ambae ndie mpenzi wake wa sasa.

Linah asema ameamua kufanya ivo ili apambane zaidi kwenye muziki kama wengine wasanii wa kike wa East Africa.

Ameongeza kua bado yeye na kundi lake “SIKILIZA BAND” hawajasambaratika bali tu wameamua kufanya kazi kila mmoja kivyake ili wajitanue zaidi na waweke mchango mkubwa kwenye muziki wa Burundi.

Alipo ulizwa kwamba kuna faida atakayo ipata akifanya muziki kivyake bila vivi, Linah amejibu.

“” Yah faida ipo na kufanya muziki peke yangu inanipa full control of my career… Uamuzi wakufany kitu flani kwa wakati gani na kwa style ipi… Ambae ni tofauti sana nikiwa pamoja na wengine… It just makes me perform according to my own speed“, amesema Linah Blanche.

Itazame hapa ngoma aliofanya na Vivi Muyomba inayoitwa “Sema” :

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com