NGM257

Masterland atangaza kusitisha uzinduzi wa Album yake

Spread the love

Masterland ametangaza kusitisha uzinduzi wa album yake iliyopewa jina la EGO asubuhi ya Jumatatu, tarehe 2 Aprili 2019

 

Mwanamuziki huyo na Mkurugenzi wa Master-Muzik ametangaza habari hiyo kupitia barua iliyosomeka kama ifuatavyo:

“Nawafahamisha ya kwamba tamasha linalosubiliwa na watu wengi na mimi nikiwemo la kuzindua Album yangu ya “EGO” ambalo lingefanyika tarehe 21 Aprili 2019 kwenye viwanja vya Lacosta Beach limesitishwa.” Ameandika Masterland

“Sababu kubwa hasa ni kuwa tunahitaji kuwapa vitu vikubwa kama tulivyowaahidi, tunaona bado hatujaeneza kila kinachohitajika. ila hadi muda huu tushakamilisha 60% za maandalizi.” Ameongezea Masterland

“Tarehe mpya mtazifahamishwa siku za mble muda si mrefu. Maandalizi yanaendelea kama kawaida yetu kwa pande zote.

“Tunaomba mtuelewe, mtusamehe pia mtumaini maandalizi mazuri ndani ya Tamasha hilo” Alimalizia Masterland

Tamasha hilo la uzinduzi wa Album yake ya kwanza iliyopewa jina la “EGO” lingefanyika Tarehe 21 April 2019 kwenye viwanja vya Lacosta Beach huku wasanii nguli kwenye tasnia ya Muziki wa Buja Fleva wakitumbuiza siku hiyo.

Tamasha la NGOZI latajwa kuwa Sababu

Tangazo la Masterland kusitisha Tamasha hilo la Uzinduzi wa Album yake limeibuka asubuhi ya tarehe 2 April baada ya kuwa kuna Chapisho la Tamasha ambalo litamhusisha Masterland mwenye akiwa na Rally mkoani Ngozi, Tarehe hizo hizo 21 April 2019. Na hii imeibuka kama sababu kwa baadhi ya mashabiki wake.

Masterland alikanusha na kusema: “ Hapana, hapana, hapana kabisa”

“Tamasha la Ngozi Ngozi siyo sababu ya mimi kusitisha uzinduzi wa Album yangu. Hiyo ni tofauti sana.

“Uzinduzi wa Album yangu ni kitu kikubwa ambacho kinahitaji muda mwingi sana wa maandalizi. Mi mwenyeye niko kwenye kamati ya waandaji wa tamasha hilo ya Ngozi, hivo siyo sababu.”

NGM itaendelea kukufahamisha chochote kitakachofuata kutoka kwa mkali huyo wa nyimbo kama Sabwe, Nzobikora na zinginezo ili aelezea sababu zaidi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com