NGM257

Mbwembwe za ujio mpya wa Black G kwenye muziki zawatia presha wasanii Burundi

Spread the love

Baada ya kimya cha muda mrefu kwenye game la muziki Burundi, jina la msanii Juma Marembo a.k.a Black G sasa laanza kupamba moto kila kona ya Burundi.

Mbwembwe za ujio wake kwenye bujafleva zimeanza kusikilizika baada ya msanii huyo kusaini mkataba wa kikazi za muziki na label ya Light Entertainment Company iliyokuwa ikizisimania kazi za msanii Sat B.

Label hiyo ya LEC imeamua kumrejesha kwenye game Black G kwa kishindo kikubwa ambapo mbwembwe tu zamatangazo bila wimbo za ujio wake zimeanza kuwaweka roho hewani mastaa kibao kwenye muziki wa Burundi maana wengi wanajua uwezo na kipaji chake kwenye muziki.

LEC imetinga camera zake kila kona ya bujumbura na ku shoot short videos kama matangazo ya ujio wa Black G uku wakitumia Hashtag #BlackIsBack.

 

Media nyingi za East Africa na za Burundi zimeanza kuzungumzia ujio huyo mpya wa Black G uku baadhi ya wasanii na mashabiki wa bujafleva wakifurahishwa pia na ujio wa Black G kwenye game la muziki.

“GIVE ME LOVE” ndio jina la ngoma ambayo staa huyo ataachia hivi karibuni Na ngoma hiyo inasemekana imesukwa vizuri na Producer Lizer wa Wasafi Record, Black G athibitisha hilo kupitia kurasa zake za instagram.

Ikumbukwe kwamba label ya LEC kwasasa imewakusanya wasanii kama Kebby Boy na Black G ni baada ya kumwagana vibaya na msanii Sat B.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com