Meneja wa Trust Nobody Wanda Boy atua Buja na kauli ya kuchafua

Spread the love

Wanda Boy mmiliki wa lebo ya mziki nchini inayotambulika kwa jina la Trust nobody alitua Bujumbura hiyo jana (januari 22,2019) kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jijini humo .

Katika zile kauli ambazo alizitoa kipindi alikua akipokelewa na waandishi wa habari mbali mbali pamoja na mashabiki wa mziki wa Buja fleva ni kwamba amekuja kuchafua kwenye game hii ya +257 hilo limesikika pindi alikua akijibu haya na Yale kuhusiana na ujio wake wa kufungua studio ya lebo yake pia kumleta moja kati ya maproducer wakali East Africa anaebeba jina la Iyogo on the beat

Ikumbukwe kwamba siku zilizopita ilikuepo ghasia kati ya lebo hii na moja kati ya wasanii waliokua wakishirikiana nao kufanya kazi nae si mwingine ni Sat B. Ikumbukwe pia kama Msanii huyo amerikodi wimbo na moja kati ya wasanii wakubwa nchini Rwanda anaetambulika kwa jina la Meddy ila rikodi hiyo bado haijaachiwa na msanii huyo kashatoka rasmi kwenye lebo hiyo wakati huo pia wimbo huo ukiwa umebaki na lebo hiyo ya Trust nobody

Tunasikia kama anakuja kuchafua, tusubiri kuvujishwa kwa wimbo huo kama ilivyofanyika kwenye nyimbo zingine kama Karabarya au tusubiri kazi nyingine za wasanii wanaotumika na lebo hiyo?

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat