NGM257

NATACHA atua Bujumbura kwa kishindo,apagawishwa na mapokezi(VIDEO)

Spread the love

Mwanamuziki wa kizazi kipya ,NATACHA LA NAMBA, LA BOSS ametua mjini Bujumbura baada ya kushinda tuzo ya mwanamuziki aliyependwa sana na mashabiki Afrika nzima, Moja kati ya vitengo vya tuzo za HIPIPO kutoka Uganda.

NATACHA ametua mjini Bujumbura majira ya saa tatu na nusu za asubuhi,akiwa amesubiliwa na umati wa watu wengi kwa ndelemo na vigelegele kwa wingi wakiwemo mashabiki wake ,wapenzi wa muziki wa Burundi, na watangazaji kutoka vituo vya Radio na TV mbalimbali vya Burundi.

Ashinda moja kati ya tuzo za HIPIPO MUSIC AWARDS UGANDA

Mwanamuziki huyo ameweza kushinda moja kati ya tuzo za HIPIPO MUSIC AWARDS zilizofanyika nchini Uganda jumamosi,16 Machi.

NATACHA ameshinda tuzo hiyo kwenye kitengo(Category) cha Mwanamuziki aliyependwa sana na mashabiki zaidi Africa (Africa Fans Favorite Fresh Talent). Ameshinda baada ya kuwapiga chini wasanii kutoka Nchi tofauti za Afrika kama MBOSSO kutoka Tanzania, KING MONADA kutoka SOUTH AFRICA,na wengine kutoka Kenya na Nigeria.

NATASHA awashukuru wote waliomchagua

Kupitia mahojiano(INTERVIEW) akizungumza na watangazaji na waandishi wa habari uwanja wa ndege, NATACHA ameshukuru sana kila mtu ambaye alimchagua na kumuwezesha kushinda tuzo hiyo.

“Ninayo furaha kubwa sana mpaka sijui nitaielezaje.” alisema NATACHA

“Nashukuru kila mtu ambaye alinichagua, nashukuru vituo vyote vya radio na televisheni kwa kuniunga mkono na kuitangaza sauti yangu na kuwezesha watu kunichangua. Sina cha kuwalipa ila nashukuru sana.” Aliongezea

“Nimeshinda hii tuzo lakini siyo mimi tu,

“Hii tuzo ni ya mashabiki wangu, wapenzi wa muziki wa Burundi, na ni heshima pia kwa Nchi yangu ya Burundi.”

Wanaoandaa Tuzo Burundi wajifunze kupitia wengine

Alipoulizwa kuhusu utofauti ambao ameuona kati ya Tuzo za HIPIPO na Tuzo ambazo zinaandaliwa Nchini Burundi, Natacha amefunguka na kusema: “Wanaoandaa Tuzo Burundi inabidi kwanza watembee waone na wajifunze jinsi gani nchi ziingine wanaandaa tuzo zao”

“Wasikurupuke kuandaa vitu ambavyo havimpi thamani na heshima mwanamuziki,vitu ambavyo vinaturudisha nyuma.” aliongezea

Aahadi kufanya wimbo mwingine na Msanii mkubwa Afrika tena

Baada ya kuulizwa kuwa kuna wimbo wowote ambao anatarajia kuutengeneza baada ya kukutana na wasanii kutoka nchi tofauti za Afrika. NATACHA alijibu: “Unajua mimi siyo mtu wa kuharakisha vitu, mambo yangu yote yanaenda kwenye mpangilio na muda wake pia”

“Kazi mpya nitaifanya na msanii mkubwa wa Afrika lakini hapana wa Afrika Mashariki, sababu nishafanya na wasanii wengi wa Afrika Mashariki”

“Watu wategemee tu kama kazi itafanyika na Msanii mkubwa tu< lakini itakuwa SURPRISE siwezi nikamsema jina” alimalizia NATACHA

Msafara wake utikisa Mji wote wa Bujumbura

Baada ya kumaliza mahojiano na watangazaji na waandishi wa habari, Natacha na msafara wake wote wameweza kuzunguka sehemu tofauti ambazo zinauunda mji wa Bujumbura  wakionyesha Tuzo ambayo ameshinda. Wamezunguka mpaka kwenda anapoishi mama yake mzazi JABE.

NATACHA na msafara wake mjiniBujumbura kati| Picha : NGM TV257

Tazama Mahojiano(INTERVIEW) ya NATACHA uwanja wa Ndege wakati anawasil

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com