NGM257

News : Aimé Loveness kuachia wimbo mpya ?

Spread the love

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Aimé Loveness ambae alifahamika sana katika kundi la muziki Mirror Team, atarajia kuachia wimbo mpya pekee yake baada ya kuona anaweza kujitambulisha vizuri akiwa nje kama ndani ya kundi.

Aimé alisema mwaka wa 2018 ni mwaka wa kujitambulisha na kwamba ana imani mwaka 2019 una kila dalili za kuwa na neema huku akiwa anakamilisha kuachia wimbo mpya.

”mwaka huu 2018 una historia kwangu na ulikuwa mzuri kwa watu wote, kwa hiyo siwezi kuacha kumshukuru Mungu, mwaka huu nimefanya mabadiliko kwenye kila kitu, kwenye nyimbo, video na utunzi. Nitaachia wimbo mpya ambao nimetumika na Master Land ndani ya Master Music Record.  Hakika wimbo utaupenda na kila anaeusikiliza kionjo anasema utakua moto wa kuotea mbali”. Alisema Aimé Loveness.Kazi yake ya kwanza akiwa nje  ya kundi hii hapa :

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com