NGM257

News: Big Fizzo kamchana nani kwenye ngoma yake mpya itakayo kuja soon.

Spread the love

Maswali ni mengi sana baada ya Big Fizzo kupost kipande cha ngoma yake mpya ambayo msanii huyo anasema itatujia hivi karibuni.

Kwenye kionjo hicho kilicho postiwa kwenye kurasa zake za instagram na staa huyo yamesikilizika maneno yasemayo “Watapata tabu sanaa”.

Maneno hayo yameishaanza kuleta gumzo mtandaoni na mitaani na watu wanajiuliza nani amepingwa kombora hilo baada ya lile la Konzi.

Baada ya muda mchache Big Fizzo aliposti picha yake kwenye kurasa zake za Twitter na Facebook na kuweka caption isemayo:”Hari Grenade ishaka itegwe muri bujafleva, ni bande izohitana ? Tuyitere canke turindire?”

Apo akimaanisha kwamba “kuna kombora linataka kurushwa kwenye muziki wa Bujafleva, je ni nani litakae mpitua?”

 

Kwenye ngoma hiyo imesikilizika kwamba itakuwa ngoma yenye miondoko ya Traps ao Slaps.

Hii inakuja baada ya ile ya Konzi ilioleta mtafaruko kati ya wasani mbali mbali wa bujafleva na kuleta kutengana katiyake na msanii mkongwe Lolilo na SatB ambae kwasasa amekuwa ndie mpinzani wake mkubwa kwenye muziki wa Burundi.

Itazame hapa Konzi by Big Fizzo:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com