NGM257

News | Burundi tunavipaji kuliko bongo ila tatizo kujiendeleza, asema Kingorongoro

Spread the love

Magic Soldier a.k.a Kingorongoro ni rapa mkali Burundi, baada ya kuwa na hit mbali mbali nchini na kuaminika nje ya nchi, management yake mpya TRUST NO BODY PRODUCTION ilimpeleka Tanzania kwa kazi zaidi.

Katika ziara yake hiyo nchini Tanzania Kingorongoro alifanikisha kufanya kazi chache na wasanii wa Bonbo Fleva ambazo anatarajia kuziachia moja baada ya nyingine siku za Mbele.

Katika maojiano na waandishi wa habari nchini Burundi, hitmaker wa wimbo Vunja Goti, Kingorongoro alifunguka na kusema kwamba wasanii wa Buja Fleva ni bora zaidi kuliko wa bongo fleva kwa upande wa kufanya muziki Live na kuongeza kuwa wasanii wa Buja Fleva wanavipaji ya kuimba na kutunga pekee yao kuliko wa Bongo ila tatizo kujiendeleza.

Aidha, Rapa huyu anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake hivi karibuni aliyomshirikisha msanii wa Bongo Fleva anayezidi kufanya vizuri kwasasa nchini hapo, Barakah The Prince, aliwataka mashabiki wa muziki wasubiri kwa hamu ujio wake mpya huku akimalizia na kusema kwamba muziki ni biashara na anajua mashabiki wanapenda kuona mchanganyiko wa watu tofauti, kwasasa imetokea kama mazingira ikiendelea kuwa sawa atafanya collabo na wasanii wa Nigeria pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat