NGM257

News: Étoile du Centre waibuka tena na RWASAZE, ni baada ya kimya kirefu.

Spread the love

Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye kundi kongwe la muziki wa Buja Fleva, Étoile du Centre limerudi tena rasmi kwenye ramani ya muziki huyo.

Kundi hilo lenye wanamuziki wanne ambao ni Willy, Romeo, Paci na Dj Daddy, lilijizolea umaarufu mkubwa katika anga ya muziki wa Buja Fleva miaka ya 2000 kutokana na uhodari katika uimbaji.

Mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo Willy amesema kuwa walikuwa kimya kutokana na majukumu tofauti, lakini wameona kiu ya mashabiki imekuwa kubwa na hivi karibuni wataachia kibao kitakachoitwa ‘Rwasaze’ kilichopikwa vizuri na producer Amir Pro na kwenye ngoma hiyo atasikika Willy na Paci.

 

Willy ameongeza kuwa wameamua kurudi tena kwenye game ya muziki wa Buja Fleva kutokana na maoni ya mashabiki wao kuwataka kurudi kwenye muziki huo baada ya kukosa huduma ya wasanii hao kwa muda mrefu.

Willy amesema pia wamekuja kuleta ladha tofauti ya muziki ili kuleta changamoto zaidi kwenye game la muziki wa Buja Fleva.

Ikumbukwe kwamba kundi hili likijengea umaarufu mkubwa kupitia ngoma zao kama : Fata Taxi, Dangerous, Izere,..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com