NGM257

News: Gavana wa Rumonge Juvenal Bigirimana awakubalia zawadi nono wane wakwanza wa Izere Awards 2018

Spread the love

Baada ya kituo cha Redio izere Fm kuandaa na kugawa Awards kwa wasanii wa mkoani Rumonge septemba 1st, Gouvernor wa mkoa huyo Juvenal Bigirimana awakubalia wasanii wane wa kwanza zawadi nono kama kuwatia nguvu wasanii hao kwenye kazi zao za muziki.

Wasanii waliojinyakulia pesa ni wane pekee kwa wale kumi na tisa waliowania.

Wakwanza alikuwa Bimenyimana Pancras (Tisa Ronick) kupitia wimbo wake Sikobizohora alipewa milion moja pesa za Burundi (1,000,000 Fbu), wapili ni Arnaud Ndayishimiye(Arnovic) na wimbo wake Pole Pole alipewa 700.000Fbu, watatu Nivyayo FayIsaie (Famous) na ngoma yake Ikibajou alijinyakulia 400.000Fbu na msichana pekee kwenye mashindano hayo Ninahazwe Choisilène (Nina Burundi) alichukuwa nafasi ya nne kupitia ngoma yake Ur’Uw’agaciro na akapewa 200.000Fbu.

Juvenal Bigirimana amesema kwamba amefurahishwa na kitendo cha Radio Izere Fm kwakuwasapo vijana wenye vipaji mkoani humo iliwajiendeleze kwenye kazi zao za muziki, aliongeza kwamba wane wa kwanza atawapa zawadi kama wasani wakubwa kwenye mkoa huyo wa Rumonge.

Ikumbukwe kwamba hii ni award ya pili ambayo imeandaliwa na kituo hicho cha Redio Izere Fm na yakwanza alipewa Msamalia Danielo.

 

Na huu ndio wimbo ulionyakuwa nafasi ya kwanza mwaka huu kwenye Izere Awards 2018

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com