NGM257

News | Licha ya idadi kubwa ya wasanii ila wengi HAWAFAHAMIKI, hii ndio sababu

Spread the love

Naam kitu kInachoshangaza wengi na kutufanya tusielewe kuhusu sanaa yetu ya Burundi ni kwamba tuna idadi kubwa ya wasanii lakini wengi hawafahamiki, hivi wajua nini tatizo?

Hii ni swali ya kujiuliza na kujaribu kuchunguza kila upande, utakuja kupata kila mmoja anamlaumu mwingine. Ni takribani sasa miaka miwili au mitatu sasa hatuna wasanii wapya kwa idadi yenye kuridhisha, wasanii wengi wanaosikika ni wale wale waliokuwepo tangu awali (Fizzo, Sat B, Lolilo, Happy Famba  na Natacha).

Sababu ni nyingi zinazotajwa, ikiwemo wasanii wapya kutokupewa fursa au promo na vyombo vya habari na nyingine sababu sugu inayotajwa ni rushwa inatajwa kuwa kikwazo na kingine wasanii wapya wanakosa fikra ya kuungana mkono na wasanii waliotangulia.

Msanii kama Fizzo na Lolilo walitoka walipoanza muziki kila mmoja na wakati wake walijaribu kuwa tofauti na wengine wote waliowakuta kipindi kile, kila mmoja alikuja na ladha yake ya kipekee.

Msanii Sat B ambaye kwasasa anazidi kupata sifa kila kukicha kupitia  muziki wake na hauwezi kuwa mubishi kwamba mashabiki wa muziki wa ndani na nje ya Burundi hakika wameshindwa kujizuia kumkubali Sat B.

Unajua sababu kubwa na ya msingi ni wasanii wanaochipukia (wapya) KUIGA AU KUFANYA YALE YALE AMBAYO YAMESHAFANYWA NA WASANII WALIOTANGULIA AO WALIOPO, huku wengine wanajaribu kuiga kila kitu mpaka sauti ya wasanii wa nje.

Utakuta msanii wa Burundi anataka kusikika kama fulani, anaimba kwa mtindo wenye kufanana kabisa labda na Diamond, Sat B,  Fizzo wengine wanataka kufanya hip hop kama T Max, Jay Kizzo mpaka shabiki anapatwa na kigugumizi aelewi ni nani aliyeimba wimbo husika.

Hauwezi kufika popote kwa kuiga msanii ambaye tayari alifanya vizuri mbele yako bali utabaki na sifa ya hapo hapo ulipo mtaani kwenu ila kitu muhimu unapashwa kuiga chipukizi ni JINSI YA KUFANYA KAZI BORA YA SANAA PIA MTINDO WAKO WA MUZIKI NDIO UTAMBULISHO WAKO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com