NGM257

News | Nelson B kuangukiwa na neema hii ni funzo kwa mastaa wengi

Spread the love

Hakika mwanzo wa mvua ni mawingu, milango ya msanii wa muziki kutoka Burundi inazidi kufunguliwa kwa Nelson-B.

Baada ya kutangaziwa kusaini mkataba wa kujiunga na lebo Trust no Body (TNB) siku chache zilizlopita, msanii huyo ameonekana kuanza kuwateka viongozi wa TNB. Ilitangazwa sana nchini kuwa staa wa muziki Sat-B anatarajia kufanya collabo na nyota wa muziki kutoka Rwanda, Meddy pindi staa huyo wa Burundi alikuwa ndani ya lebo ya TNB.

Kwa mjibu wa kiongozi wa TNB, Wanda Boy maarufu kwa jina la Mzee Baba alichukuwa maamzi ya kumfuta Sat-B kwenye arakati nzima ya collabo na Meddy na kumuweka Nelson-B nafasi hiyo.

“Kiufupi munajua kwamba hiyo collabo iko chini ya mikono yangu, so ni lazma nimefanya mabadiliko kidogo ya kumchukua Nelson-B, na kumuweka nafasi ya Sat-B na kitu kinatoka. Meddy ni msanii mkubwa na kiufupi alielewa kuwa hatuhitajii wa kosa adabu kwenye muziki, muziki unahitaji adabu, sisi tunafanya kazi” althibitisha hayo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Ngm257, Nelly Natt.

Moja ya kazi ya Nelson-B hiyi hapa :

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com