NGM257

News | Sababu kubwa ya Black G kuimba na Big Fizzo

Spread the love

Msanii aliyekuwa na nyota kubwa ya kupendwa na wasichana katika game la muziki wa kizazi kipya, Black-G ambae alikuwa kimya kwa kipindi cha muda mrefu ametangaza kuja na ujio mpya huku akitarajia kufanya kazi na moja ya wasanii wanaofanya vizuri sasa katika soko la muziki, Big Fizzo na anaamini kuwa itakuwa kazi nzuri.

Black- G ambae alikuwa akitamba sana kipindi cha nyuma na nyimbo zake kama Babiri Babiri, Oya, Urihe, Sivyiza na nyingine nyingi alizofanya na wasanii wenzie wakubwa.

Kwasasa anakaribia kuingia sokoni tena kwa kishindo na moja kubwa ya sababu kwanza, inaonekana anawamiss mashabiki zake, pili anamiss zile sifa kipindi kile.

Sababu nyingine kubwa ya Black G kuwa na kiu ya kuimba na Big Fizzo kwa sababu yeye na Big Fizzo sio wasanii bali ni wanamuziki hivyo wimbo wake akimshirikisha Fizzo lazima utakuwa mzuri sana.

Kwasasa Msanii huyo anaonekana kajipanga vizuri ili kuweza kufanya vizuri.

Hata hivyo atawashangaza watu wengi kwa sababu ana mpango wa kurudi kitofauti katika muziki na hata muonekano wake pia hautakuwa kama wa mwanzo.

Hata hivyo, msanii huyo atajitahidi kurudi katika nafasi yake ila sio jambo raisi kwa sababu kuna vijana wapya wanafanya vizuri zaidi.

Kwa mtazamo wangu wa karibu nimegundua kuwa wasanii wengi wa muziki waliokuwa wamekaa kimya kwa mda mrefu wataanza kurudi katika game, hii ni kutokana kuwa MUZIKI WA SASA UMEKUWA NA MAFANIKIO YANAYOONEKANA NA UMEKUWA NI TOFAUTI NA ULE WA KIPINDI CHA MWANZO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com