News| Sat-B amwaga povu zito kwa wanaozidi kuharibu soko la muziki Burundi

Spread the love

Msanii wa BujaFleva Sat-B ni mmoja wa wasanii ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye muziki ilhali ya wasanii wengi wenye sauti nzuri kujitokeza.

Sat-B ameweza kuachia nyimbo kwa miaka mingi sasa,na bado nyota yake inazidi ng’aa.Staa huyu ndie msani pekee alieweza kuzipandisha bei za shows ilihali wasani wanufaike kupitia shows hizo na wazidi kujisaidia kimaisha na wapate pesa za kutengeneza ngoma zingine bora ambazo zitakuja kuipa heshima burundi kupitia muziki.

Sat-B amesema misingi aliyoijenga ya soko hilo la muziki kwamba kuna watu wapo wanajaribu kulivunja ili wajinufaishe wao wenyewe.

Kupitia status yake ya whatsapp Sat-B amemtolea povu mtu ambae hajapenda kumtaja jina ambae yupo anaharibu soko hilo la muziki kupitia shows,ambapo anasema mtu huyo yupo anapunguza bei za shows hizo ili Sat-B akose soko.

Sat-B ameandika ujumbe mzito :“Ndugu nimekuachia ufanye shows kwasababu nipo kwenye mwezi mtukufu wa ramadhan ,sasa umeanza kuharibu bei za shows ilimradi uniharibie na uharibu misingi niliyoijenga. Sasa unayoyafanya ninayaona na unapotaka kuniharibia tayari nimeshapagunduwa ila nakusihi kwamba hutoweza, we subiria tu mwezi mtukufu wa ramadhan uishe utaona”.Ameandika Sat-B.

Mkali huyu wa “Feel Love’’ anaendelea kutisha kupitia nyimbo zake na ivi karibuni ataachia collabo aliyofanya na msanii wa Bongofleva Dully Sykes ambapo ngoma tayari imepewa jina “Girl Friend“,ngoma iyo imewakusanya ma producer kutoka Burundi na Uganda “Kolly The Magic na Nessim“. Yote hayo Sat-B anasema ni kwasababu anajuwa wanachotaka mashabiki wa muziki wa BujaFleva na anataka kuuona muziki wa burundi unazidi kuvuka boda zaidi.

Endelea kufuatilia tovuti zetu za www.ngm257.com tutakujuza mengi kuhusu ngoma yake iyo mpya aliyoshirikiana na msani wa Bongo Dully Sykes.

Related Post

You May Also Like

One thought on “News| Sat-B amwaga povu zito kwa wanaozidi kuharibu soko la muziki Burundi

  1. Chizi huyo, hata wauzaji wa bidhaa mbali mbali hawauzi kwa bei sawa sawa, kila mmoja huuza kwa bei yake ambayo inamnufaisha!!Sat B bado ugonjwa wa Cancer unamsumbuwa sio Bure!!aache kujikuza, atambue tu kama yeye ni mdogo saana tuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat