NGM257

News | Tambwe Remy kushirikiana na kufanya kazi na NIHO TV

Spread the love

Muigizaji maarufu wa Burundi Movie akiwa kiongozi wa kundi la filamu nchini la Tambwe The Great Film (TGF), Tambwe Remy akifahamika sana kwajina la Mr Comedylogy, apewa nafasi ya kushirikiana rasmi na NIHO TV  inayomilikiwa na Pasteur Bagenzi.

Muchekeshaji huyo ambaye alifanikiwa kushinda tuzo ya Soft Media amekuwa wa kwanza kutia saini ya kushirikiana na kufanya kazi na NIHO TV kama Brand Patner na pia ni mmoja wa waigizaji  wa Burundi walio katika program ya Uchekeshaji (Comedy) unaopendwa zaidi Burundi hata Afrika Mashariki.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa NIHO TV alionesha furaha yake ya kushirikiana na Muigizaji  mwenye kiwango kama Tambwe na kuongeza kwamba ni hatua nzuri kwa tasnia ya filamu nchini.

NiHO TV imehakikisha kwamba wapenzi wao wataendelea kupata Comedy bora ya Afrika inawafikia pale walipo na watafanya kazi na na Tambwe (Mr Comedylogy) kwa kupanua wigo wa wateja wao na itakua ni moja ya fursa ya kutangaza tasnia ya filamu nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com