News| UKEBURWATAN inatarajia ku lanchi filamu mpya Februari 22

Spread the love

Kampuni ambayo inajihusisha na mambo mengi Afrika Mashariki, UKEBURWATAN inayo ongozwa na mwana mama Ndayirorere Suavis kwajina maarufu Amina, inatarajia ku lanchi filamu mpya mwishoni mwa mwezi Februari, 22 kwenye ukumbi wa Hoteli Source du Nil.

Baada ya kiongozi huyo kutembelea baadhi ya mikoa nchini Burundi na kugundua vipaji vya waigizaji wa filamu nchini Burundi, iliweza kumpa nguvu na bidii ya kuendelea kupambana mpaka pale tasnia ya filamu irudi kwenye kiwango kinacho ridhisha kama zamani.Muigizaji maarufu nchini kwa upande wa wanawake, Ndayirorere Suavis alitufungia na kusema hayo wakati akifanya mahojiano na muandishi wetu na kutuonesha kipande cha movie hiyo aliyoipa jina la  “Ukundahuza Kw’Indimi”(lugha ya kirundi) ikiwa na theme ya kuelimisha jamii lakini pia sanaa ya uchekeshaji ikiwa imehusika ndani yake.

Filamu hiyo inatarajiwa kuachiwa Tarehe 22 mwezi Februari na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo, Raisi wa Burundi, Wabunge, Mabalozi, viongozi wa ma kampuni, Radio, Televisheni na hoteli  na wageni kutoka Rwanda, Uganda, Tanzania Pamoja na Nchi ya Kenya.

Aidha, Utofauti mwingine uliopo katika Movie hiyo ni waigizaji ambao wameshirikishwa ndani yake kama vile mchekeshaji Mathematique pamoja na watoto wa tatu huku ikiongozwa na Waandaaji wa Filamu wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza movie hapa nchini.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat