NGM257

News | Vichou kuachia album mbili mwezi Desemba kwa mpigo

Spread the love

Msanii wa muziki  wa Bujafleva anayewakilisha kundi nzima la Peace & Love, Vichou Love atarajia kuachia album zake mbili kwa mpigo mapema Desemba, 16 mwaka 2018.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye mahojiano leo Novemba 18, kwenye ukumbi wa Star Hotel, mkali wa ngoma Kugatumba aliyomshirikisha msanii wa kike wa Bongo Fleva Lady Jay-D,  Vichou alisema fans wa muziki wa Afrika Mashariki na dunia nzima wategemee album zake mbili ambazo zitakuwa kwenye mtindo au miondoko kama wanavyomfahamu zikiwa zimeshiba track kibao ndani yake.

Vichou Love ametangaza rasmi ujio wa album zake mpya mbili zikifahamika kwajina la Story na Ndagukumbuye  zitakazoachiwa Desemba 16 kwenye show inaobeba jina la Ata Umunyamahanga Birashokoba kwenye ukumbi wa Lacosta Beach.

Moja ya kazi yake mpya tazama hapa :

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com