NGM257

News:Huyu ndie “Cycy La Rossy” anaekuja kuwatetemesha wasani wa kike ndani ya bujafleva.

Spread the love

Jina la kuzaliwa ni Cyntia Kanyana ila umaarufu anao kupitia jina la “Cycy La Rossy” akiwa ni miongoni mwa wasani wa kike Burundi anaekuja kwa kasi ya ajabu baada ya kufanya bonge la ngoma ” Go Down” yenye miondoko ya Afro-dancehall.

Alirikodi ngoma yake ya kwanza mwaka wa 2016 na ngoma hiyo ilipewa jina “Mfise Irungu”,baadae aliachana na muziki kidogo maana wazazi wake walipendelea asome kwanza na mwaka huyo Cycy La Rossy alijielekeza nchini Uganda ili aendeleze masomo yake.

Mwaka huu wa 2018 ndipo ameamuwa sasa kujingiza rasmi kwenye muziki baada ya kuachia ngoma yake mpya “Go Down” ambayo inaonyesha uwezo wake mkubwa wa kuimba.

La Rossy amesema kwamba huu ni mwaka wa kazi baada ya kazi na yuko na collabo nyingi na mastaa wa muziki nchini burundi ,pia ngoma hizo zinauwezo mkubwa kwaio anasema kwamba amekuja kuwatetemesha wasani wengine wa kike ndani ya bujafleva ili wafanya kazi zaidi maana wengi nikama vile wamezubaa kufanya muziki na ni muda mrefu sasa wadau wa muziki hawazioni kazi mpya za wasani wa kike.Amesema La Rossy.

Na kama bado hujaisikiliza ngoma yake mpya “Go Down” bonyeza link hii:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com