NGM257

Ole Gunnar Solskjaer atangazwa kuwa Kocha rasmi wa Manchester United

Spread the love

Ole Gunnar Solskjaer ametangazwa kukabidhiwa kandarasi ya kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu ili kuiongoza na kuifunza klabu ya Man United.

Ole Gunnar Solskjaer  ambae ni raia huyo wa Norway mwenye miaka 45,  alipata kazi Old Trafford kama kaimu mkufunzi mnmo mwezi Disemba baada ya aliyekuwa Kocha wa Klabu hiyo Jose Mourinho kufutwa kazi.

Kocha huyo ataiongoza Klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka mitatu.

Solskjaer kwa historia yake, aliichezea timu hiyo ya Manchester United misimu 11 na alifunga goli la ushindi katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya 1999.

Manchester wametangaza habari hiyo kwenye tovuti yao ikisomeka : “Manchester United inatangaza kuwa meneja wa sasa na mchezaji wa zamani, Ole Gunnar Solskjaer, amechaguliwa kuwa meneja wa muda wote wa klabu mkataba wa miaka mitatu. ”

Solskjaer aelezea furaha yake baada ya kukabithiwa rasmi klabu hiyo

”Hii ndio kazi ambayo imekuwa ndoto yangu na sasa nafurahi sana kuweza kuifunza klabu hii kwa muda mrefu”, alisema Solskjaer.

Kutoka siku ya kwanza lipowasili hapa, nilihisi nyumbani kwa klabu hii maalum, “alisema Solskjaer.

“Ilikuwa ni heshima kuwa mchezaji wa Manchester United, na kisha kuanza kazi yangu ya ukufunzi hapa. Miezi michache iliyopita nilipata uzoefu wa ajabu na nataka kuwashukuru makocha wote, wachezaji na wafanyakazi kwa kazi tuliyofanya hadi sasa. Ni zaidi ya msisimko kupata nafasi kubwa kama hii ya kuongoza klabu ya muda mrefu na nina matumaini kuifikisha kwenye mafanikio makubwa ambayo mashabiki wetu wanayositahili.” Aliongezea Solskjaer.

Kiongozi msaidizi wa Klabu ya Manchester United , Ed Woodward ampongeza Ole

“Nachukua nafasi hii kumshukuru Ole na uongozi wote wa mafunzo ya Klabu yetu kwa kazi ambayo wameshaifanya, ninampongeza pia kwa hatua nyingine ambayo amefikia kukabidhiwa kuongoza Klabu hii. Mashabiki na kila mtu kwenye Klabu tuko nyuma yake kama anavyoonekana kutufikisha tunapotaka ili kuendelea kuijenga historia ya timu yetu.” Alisema Ed Woodward.

Ikumbukwe kuwa, Solskjaer ndio meneja wa kwanza wa Man United kushinda mechi sita za ligi mfululizo akivunja rekodi iliowekwa na Sir Matt Busby.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com