NGM257

PRIMUSIC yafunguliwa tena kwa kishindo, 25.000.000BIF zatengwa kwa mshindi.

Spread the love

PRIMUSIC 2019, Shindano la kusaka vipaji nchini Burundi larudi kwa kishindo baada ya miaka 5 likiwa limesimamishwa, milioni 25 za pesa ya Burundi zatengwa kwa mshindi wa kwanza.

Baada ya muda mrefu likiwa limesimamisha, shindano la PRIMUSIC ambalo huandaliwa na kampuni ya kutengeneza pombe nchini Burundi limeweza kuzinduliwa tena alhamisi, 19 Mei 2019 kwenye mijengo ya kampuni hiyo.

Shindano hilo ambalo hukusanya vipaji vyote kutoka mikoa yote ya Burundi litaanza rasmi alhamisi ya 23 mei 2019 mkoani Kayanza.

BIG FIZZO na SAT B wateuliwa kama mabarozi wa PRIMUSIC

Wakali wa Buja fleva,B FIZZO na SAT B wameweza kuteuliwa kama mabarozi wa shindano hilo, na watapata nafasi kubwa na kuzunguka na timu nzima ya PRIMUSIC kwenye mikoa yote ya Burundi na kuburudisha rai ambao watahudhuria shindano hilo.

NATACHA akosa nafasi ya ubarozi

NATACHA ni miongoni mwa wanamuziki ambao walitegemewa sana kuoneka kwenye shindano hilo kama barozi pia, lakini uongozi wa PRIMUSIC umeweza kuweka wazi na kusema: “Tulitamani sana kuwa na barozi wa aina zote wakike na kiume na NATACHA ni mmoja kati ya watu tuliowatazama sana na kuhitaji kuwa nao, lakini hatukuweza kuelewana.” alisema Dorine Gatena Mkurungenzi mzarishaji wa PRIMUS

Mshindi wa kwanza kuibuka na kitita cha 25.000.000BIF

Fainali za PRIMUSIC zitafanyika mjini Bujumbura mwezi July 2019, msanii kutoka nje ya Burundi ambaye hakutajwa jina atashiriki kuwaburundisha wananchi wa Burundi.

MshindI wa kwanza ataibuka na kitika cha milioni ishirini na tano pesa za Burundi (25.000.000BIF), huku mshindi wa pili akipata 5.000.000BIF, mshindi wa tatu atapewa 3.000.000BIF, wa nne najipatia 2.000.000BIF, wa tano atapata 1.500.000BIF ,huku mshidni wa sita akienda na 1.000.000BIF.

Jinsi ya kujiandikisha

Mtu yeyyote ambaye anajuwa kuwa ana kipaji cha kuimba, anakaribishwa kujiandikisha ili kushiriki shindano hilo.

Mshiriki anaweza kujiandikisha kupitia ukurasa wa Facebook wa Primus, au kwenye wavuti (Website) ya Primus na kupitia Application ya Primus Mobile App.

Wasanii wanaofanya HIP HOP wawekwa mashakani

Shindano hilo ambalo huwachanga wasanii wa aina zote ukianzia wanaoimba na wanaofanya mitindo ya HIP HOP, limeonekana kutowapa nafasi kubwa ya ushindi wasanii wanaofanya muziki wa HIP HOP.

Wakiulizwa kuhusu nafsi ya wasanii wanaofanya HIP HOP

Gateka amejibu, “Hatumbagui mtu, kila mtu ana haki ya kushiriki na ikiwa mahakimu watamuona kuwa bora, hivyo ushindi utakuwa ni wake”

Wawili kati ya mahakimu wa shindano hilo wakiwemo Amir Pro na Kolly da Magic wameonekana kutowapa nafasi kubwa ya ushindi wasanii wanaofanya miondoko ya HIP HOP.

“Shindano hili mara nyingi huwashirikisha wasanii wanaoimba kwa sababu wao ndio huonekana zaidi kufuata sharia na vigezo vyote vya uimbaji, hivo ni vigumu sana kwa msanii anayefanya HIP HOP kupata nafasi kubwa mbere ya msanii anayeimba.” Amesema hivyo Amir Pro

“Ningependelea kama itawezekana wasanii wa miondoko ya HIP HOP waandaliwe mashindano yao maana itakuwa vizuri hata kwetu mahakimu.” Aliongeza Amir pro

“Wasanii wa HIP HOP mara nyingi hufuata mdundo “Beat”, wao hawafuati vigezo vya muziki na kuvitendea haki kama wasanii wanaoimba, kwa hiyo hili husababishwa wasipate nafasi kubwa ya ushindi.” Alisema Koly da Magic

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com