Sat B ajiwekea rikodi ya kipekee kwenye muziki wa bujafleva, alamba laki tano za viewers uko YouTube.

Spread the love

Nyota ya Sat B yazidi kung’aa kwenye ulimwengu wa muziki, video ya ngoma yake “Feel Love” imeumulika muziki wake kwa kufikisha viewers 500.000.

Hii itakuwa ni moja kati ya Video za Sat B zilizopokelewa Vizuri na watu!! Katika Muda wa miezi 11 tu imeweza kutazamwa zaidi ya mara laki tano.
Katika Mtandao wa Instagram Sat B katoa Shukrani zake kwa wote ambao wameitazama video hii mpaka sasa..

Na hii ni rikodi ya kwanza kwa msanii kutoka Burundi kufikisha kiwango hiki cha viewers kwenye mtandao wa YouTube kwa muda wa miezi 11.

Licha ya Sat B kufanya nyimbo kadhaa nzuri huko nyuma lakini wimbo wake wa “Feel Love” ndio umekuwa kama umemtambulisha zaidi kwenye ulimwengu wa muziki kimataifa zaidi.

Na kwasasa boss huyo wa Label ya Empire Avenue anatamba na kibao “No Love”

Related Post

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat