NGM257

Sport | Inter Star ipo kwenye mazungumzo na Kocha Masudi Djuma

Spread the love

Kamati inayosimamia klabu ya Inter Star iliyopo nchini Burundi na Marekani inaendelea kujiimarisha kwa kuangalia ambacho wanahitaji baada ya Kocha Karumba Jean Tigana kusimamishwa, inasemekana maongezi ya chini chini imeanza kati ya kocha wa zamani wa Simba ya Tanzania, Masudi Djuma na Inter Star.

Kama pesa ndio kila kitu basi ndio kitu watakacho tumia ma boss wa klabu  Inter Star ni kumshawishi kocha huyo ambaye ni maarufu sana Afrika Mashariki na Afrika nzima kusaini mkataba na klabu yake ya zamani.

Swali inakuja, hivi kocha huyo anawezaje kukubali ofa ya timu ya daraja ya pili huku akitafutwa na klabu nyingi kubwa kubwa Afrika? hata kama kocha huyo aliwai kuichezea na kuifundisha  Inter Star miaka za nyuma,  kwasasa Masudi ana CV kubwa zaidi.

Inasemekana mda wowote Masudi atatua Inter Stars endapo atakubali ofa waliompa ambayo haijatajwa kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo msimu huu na kuakikisha timu imerudi daraja ya kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com