NGM257

Sport | Kenya yaitambia Burundi kwenye michuano ya Cecafa U17

Spread the love

Michuano ya CECAFA ya vijana wasio zidi miaka 17 (U17), ilizinduliwa rasmi leo Aprili, 14 inchini Burundi.

Hata hiVyo mashabiki walihitikia kwa wingi mkoani Muyinga kwa kuunga mkono nchi yao huku wachezaji wa Vivier Bahati walishinda kushinda vijana wa Harambe Stars, Kenya.

Licha ya kuandaa michuano hiyi, Intamba Murugamba ilishInda kujitetea kama waandalizi wa michuano ya Cecafa U17, vijana wa Kenya hawakusubiri mda mrefu katika dakika la 14, Nicolas alipata bao lake la kwanza na walikuja juu na kupata bao la pili katika dakika la 17.

Aidha, kipindi cha pili Burundi  wakaja juu na kumiliki mpira kiasi kikubwa ila bao la tatu la Kenya Lilikuja kuaribu mambo yote katika dakika la 53.

Burundi ilishinda namna ya kukabiliana na mashambulizi ya vijana wa Kenya huku hawakuwa na jinsi na kukubali bao la nne katika dakika la 83.

Kwa hiyo vijana wa Burundi walitambiwa na vijana wa Kenya kwa bao nne kwa sufuri (4-0). Kwasasa Burundi inachukua nafasi ya mwisho katika kundi ya kwanza nyuma ya Kenya, Somalia na Ethiopia.

Tuwakumbushe kwamba mechi ya pili ya vijana wa Burundi  itakuwa Mkoani Ngozi,  Aprili, 17, saa tisa na nusu (15:30) dhidi ya vijana wa Somalia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com