NGM257

Sport | Kufanya vizuri ni miujiza kwa LLB asema Kocha Mayelé

Spread the love

Klabu ya LLB kutoka Burundi itashiriki hivi karibuni michuano ya Cefaca nchini Tanzania huku safari ikipangwa wiki ijao.

Kwenye maojiano na muandishi wa habari wa Ngm257, Kocha mkuu wa timu ya LLB, Mayelé alisema hana miujiza ya kufanya vizuri katika michuano ya Cecafa kwa sababu maandalizi ni mabovu sana huku akiongeza kwamba haoni umuhimu wa timu yake kucheza Cecafa wakati hakuna pesa kama mtisha kwa wachezaji.

Kocha Mayelé alishangazwa sana na utaratibu wa shirikisho la soka nchini na kusema,

“sioni umuhimu wa kucheza Cecafa, wachezaji wanacheza hawana mtisha wowote wa nchi wakati tunawakilisha Burundi kwenye michuano hiyo, mkisubiri kupata matokeo mazuri itakua ni miujiza ya Mungu kwasababu tunasafiri kilometa nyingi kwa basi wakati mwakilishi wetu atasafiri na ndege, kwanini timu inayowakilisha nchi isafiri kwa ndege na mwakilishi asafiri na basi?”

Kwa kauli hiyo Kocha Mayelé amebainisha kuwa ana kabiliwa na changamoto kubwa zaidi na hapendi lawama kwa matokeo mabovu kwenye michuano ya Cecafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com