NGM257

Sport | Mbappé awatupa mbali Messi na Ronaldo kwa gharama duniani

Spread the love
Mtandao unaochunguza kwa ukaribu zaidi wachezaji wanao ingiza pesa nyingi kuliko wengine duniani CIES, ilitangaza orodha ya wachezaji 10 wanaoingiza pesa nyingi mwaka 2019( joueur le plus cher du monde en 2019).
 
Kwa hiyo Kylian Mbappé anaendelea kuongoza kuwa mchezaji wa gharama kubwa zaidi duniani mwaka 2019. Mchezaji huyo wa PSG na wa timu ya taifa ya Ufaransa ndie boss wa wachezaji kwasasa anakadiriwa kuwa na euri milioni 218.5, huku akiwa mbele ya mshambuliaji mwingine , Harry kane ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 200.3.
Mshambuliaji mwingine wa klabu ya PSG ni Neymar wa Brazil akikamilisha podium ya wachezaji 3 wenye gharama kuliko wengine duniani akikadiriwa kuwa na euro milioni 197.1.
Katika Orodha ya wachezaji 10, hakuna mchezaji mwengine wa Ufaransa au anayechezea Ligue 1 isipokuwa Mbappé na Neymar.
Klabu za Uingereza zinaongoza kwa kuwakilishwa vizuri na Raheem Sterling (4), Mohamed Salah (5), Romelu Lukaku (8) na Leroy Sané (10). 
Lionel Messi yuko katika nafasi ya 7 mbele ya Cristiano Ronaldo (19) akikadiriwa kuwa na euro milioni 127.2 pekee. kwa hali hii ya Ronaldo kushuka zaidi inasababishwa na uhamisho wake wa kujiunga na Juventus  Turin na umri wake.
Wachezaji wengine maarufu wa Ufaransa ambao wapatikana kwenye orodha hiyo ni pamoja na Antoine Griezmann (11) akiwa na euro milioni 155.2, Paul Pogba wa 17, Ousmane Dembelé wa 20, Aymeric laporte wa 26.
Ni wakumbushe kwamba kuna utofauti wa kuwa mchezaji wa gharama zaidi dunianni na kuwa mchezaji tajiri duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com