NGM257

Sport | Moussa Mossi (Hadji) aruhusiwa kucheza katika klabu ya les Lieres

Spread the love

Mchezaji wa zamani wa LLB na Vital’o, Moussa Mossi maarufu nchini kwajina la Hadji anaweza kucheza Ligi kuu  kama mchezaji wa Les Lieres baada ya kusimamishwa kwa mda na Kamati ya Mashindano ya soka FFB.

Hadji alisimamishwa Septemba 21 Kamati ya Mashindano ya Soka la FFB, ya kutokucheza mechi yoyote msimu huu baada ya kukutwa na hatia ya kitendo cha kusaini mkataba katika klabu mbili tofauti msimu moja.

Les lieres imeingia mkataba na mchezaji huyo kutoka  klabu ya LLB kwajili ya kuichezea timu hiyo kwenye Ligi Kuu Primus League na michuano ya kombe la Rais wakati Hadji alikuwa tayari alikwisha saini mkataba na timu iliyoshuka daraja, Inter Star.

Kamati ya Kisheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Burundi (FFB) limitaka Inter Star kumuacha Moussa Mossi kucheza katika klabu ya Les Lieres baada ya kufanya uchunguzi.Tuwakumbushe kuwa Hadji tayari amekwisha ichezea timu yake mpya Les Lieres mechi mbili (Musongati na Atletique Olympic) msimu huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com