NGM257

Sport | Moustapha Francis Njali atoa zawadi nono kwa timu yake ya utotoni

Spread the love

Nyota wa zamani wa timu ya Kiyovu Sport ya nchini Rwanda, Moustapha Francis Njali aliyejiunga msimu huu na Gor Mahia ya Kenya, alichukua mda mfupi baada ya kumaliza mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Afrika Can2019 dhidi ya Mali (1-1)  kutoa zawadi ya jezi na bahasha kwa timu yake ya utotoni Kavumu FC ya Burundi.

Njali alionesha mapenzi kwa timu yake ya zamani tangu utotoni klabu ya Kuvumu FC licha ya mafanikio anayozidi kupata kwasasa aliona ni bora zaidi kuanza kwa kumushukuru Mungu na kukumbuka mahali alipoanza.

” Sio mara kwanza natembelea nchini kila mara nakuja kwasababu nyumbani ni nyumbani na nimepata mafanikio kidogo basi nimeona chakufanya ni kurudi mahali nilipoanzia kutoa shukrani. Nivizuri unapo pata mafanikio ukumbuke mahali ulipotoka. Kavumu FC ni timu ambao imekuza wachezaji wengi na kwasasa wanaendelea sawa ila kikubwa nikukumbuka ulipotoka na kurudi kupata baraka”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat