NGM257

Sport| Mpaka kimeeleweka! Hatimae Hussein Tchabalala asaini Baroka FC.

Spread the love

Mshambuliaji wa klabu ya Rayon Sport na timu ya taifa ya Burundi, Hushein Shabani Tchabalala amejiunga rasmi na Baroka FC.

Klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini, imeweka saini na mshambuliaji mrundi Hussein Shabani Tchabalala, mshambuliaji mrefu kiasi, mwenye nguvu na ana kipaji cha kuona lango kila mara akitokea nchini Rwanda katika klabu ya Rayon Sport baada ya kuonekana katika mchezo wa Caf Champions dhidi ya Mamelodi Sundowns mapema mwaka huu.

Aidha, Tchabalala alisaini mkataba wa miaka miwili na Baroka FC baada ya kucheza michezo 10 katika timu ya Rayon Sport akiwa na bao 7 huku kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa CAF na shirikisho alifunga bao 4.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com