NGM257

Sport | Ronaldinho kafirisika vibaya sana licha ya umaarufu wake wote

Spread the love

Baada ya kutekelezwa na mahakama ya Brazil, nyota wa zamani wa FC Barcelona, PSG na AC Milan, Ronaldinho Gaucho katika akaunti yake ya benki  ana Euro sita pekee (6€).

Hakuna kinachoendelea kwa Ronaldinho tena, wakati huu anapitia katika wakati mgumu sana kama mtu anaeanza kutafuta maisha. Mwaka 2015 alishtumiwa kwa ujenzi haramu wa nyumba katika eneo lisilo ruhusiwa nchini Brazil, nambari 10 ya Seleçao alitakiwa kulipa faini ya € 2,000,000.

Bingwa wa dunia wa 2002 hakulipa faini hiyo, na haki ya Brazili ghafla ikaamua kuchukua au kuziwia pasiposti yake.

Kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Globoesporte, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa kesi hiyo pia aliingia kati ili kutatua kesi na kulipa haraka iwezekanavyo na hivyo akajaribu kurejesha fedha mwenyewe, kwa kuitumia kwenye akaunti ya benki.

Cha kushangaa, kulingana na UOL Esporte walipata euro sita tu kwenye akaunti ya benki ya nyota huyo!

Mpaka sasa Ronaldinho anadhaminiwa na kampuni ya Marekani ya Nike, bado kila mtu ajiuliza swali kwamba pesa za Ronaldinho zinawekwa wapi?

Tuwakumbushe kuwa Ronaldinho aliwai kupata mpira wa dhahabu mwaka 2005.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com