Sport | Rukinzo FC yaanza kujisuka upya, Bumamuru yaanza kudidimia

Spread the love

Klabu ya Waskari polisi, Rukinzo FC  ambayo inashiriki Ligi ya kwanza msimu huu, leo wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Messager Bujumbura katika mchezo wake wa 10 wa Ligi Kuu Primus League uliopigwa leo kwenye uwanja mkuu wa Mwana Mfalme Louis Rwagasore.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali  wa kusisimua, Rukinzo imepata mapema kutikisa nyavu za Messager Bujumbura kupitia kwa Niyunkuru Pascal dakika ya 36.

hakika mchezo ulizidi kuwa mkali ambapo Messager Buja ilipata nafasi mbili nzuri zakupata bao bila mafanikio, matokeo yalidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Rukinzo ikionekana kumiliki mpira kiasi kikubwa kuliko Messager Buja huku mechi ikimalizika matokeo yakiwa bao 1-0 kwa ushindi wa Rukinzo FC ambayo inazidi kujisuka upya baada ya kupata ushindi mechi mbili tofauti na siku za mwanzo.

Aidha, mechi nyingi leo ilikuwa ni kati ya Bujumbura City dhidi ya Bumamuru ambayo inashiriki pia Ligi ya kwanza msimu huu mchezo uliopigwa pia leo kwenye uwanja mkuu wa Mwana Mfalme Louis Rwagasore saa kumi kamili.

Vijana wa kocha Omar Ntakagero walijaribu kuondoka uwanjani na pointi tatu baada ya kupata bao 1-0 mapema sana huku Bumamuru ikiendelea  kudidimia kwa kupoteza mechi mbili katika wiki mbili.

Kocha wa Bumamuru, Thiery Nimubona amesema matokeo hayo ni mipango ya Mungu na kwamba watajipanga kufanya vizuri na kukosoa makosa madogo madogo.

 

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
WhatsApp chat