NGM257

Sport | Vital’o yaichapa bila huruma Delta Star katika fainali

Spread the love

Baada ya kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Raisi Jumamossi hii, klabu ya Vital’o imeichapa bila huruma klabu ya Delta Star ya Gatumba bao tatu bila jibu (3-0) katika fainali ya Kombe la Raisi.

Mshambuliaji wa Vital’o Issa Ngezi ndie aliyeifungia timu yake bao la kwanza katika dakika la 16, Vital’o imeendelea kuwa juu na kumiliki mpira kuliko Delta Star na kuilazimisha bao la pili katika dakika la 42 kupitia kiungo pia nahodha wao, Christian Mbirizi.

Timu ya Delta ilijaribu kutafuta kupata bao ata moja bila mafanikio katika kipindi cha pili huku kiungo wa Vitalo alikuja tenq juu na kuweka wavuni bao la tatu la mwisho katika dakika la 58.

Kwa ushindi huwo Vital’o imetwaa taji la Kombe la Raisi (2017-2018) kwa kuishinda Delta Star kwa bao 3-0 katika mchezo ulichezwa mkoani Gitega , Vital’o itawakilisha Burundi katika michuano ya shirikisho (Confederation) huku Wabingwa Messanger Ngozi itawakilisha Burundi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com