NGM257

Sports| Chelsea kuzidisha rekodi yake dhidi ya Barcelona

Spread the love

Moja kati ya michezo ya UEFA Champions League ya hatua ya 16 bora msimu wa 2017/2018 iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ni pamoja na mechi ya Chelsea dhidi ya FC Barcelona iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.

Chelsea leo walikuwa wameingia katika uwanja wao wa Stamford Bridge wakiwa nakumbuka mara ya mwisho kuifunga Barcelona ilikuwa ni April 18 2012 goli 1-0 lililofungwa na Didier Drogba dakika ya 45 ya mchezo, ukiachia ushindi huo mechi zilizofuatia zote walitoka sare.

Club ya Chelsea ikiwa nyumbani na leo imeendeleza rekodi yake kwa kupata sare yake ya tatu mfululizo dhidi ya Barcelona, baada ya kufungana goli 1-1, goli la Chelsea likifungwa na Willian dakika ya 62 huku la Barcelona likifungwa na Lionel Messi dakika ya 75, hivyo Chelsea wana kazi ya kwenda kupindua mchezo wa marudiano Nou Camp kwani ni lazima wapate ushindi au sare ya kuanzia magoli mawili.

Msimamo wa magoli ya mechi zilichezeka jana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com