NGM257

Sports| Zidane ajifufua mwenyewe Bernabeu

Spread the love

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017/2018 hatua ya 16 bora imeendelea tena usiku wa February 14 kwa michezo miwili kuchezeka, Real Madrid walikuwa nyumbani dhidi ya Paris Saint Germain ya Ufaransa huku Liverpool wakiwa Ureno kucheza dhidi ya FC Porto. Mechi ya Real Madrid dhidi ya PSG ndio ilikuwa mechi inayotajwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na PSG wamerudi Uhispania ikiwa msimu uliyopita PSG wakiwa Uhispania waliruhusu kufungwa magoli 6-1 dhidi ya FC Barcelona. Leo PSG waliingia Uhispania katika uwanja wa Santiago Bernabeu wakiwa wamejizatiti, licha ya kuwa wamepoteza tena mchezo kwa magoli 3-1, PSG ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 33 kupitia kwa Rabiot lakini Cristiano Ronaldo alisawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 45. Hali ya umiliki wa mchezo ilikuwa ni asilimia 50 kwa 50 kitu ambacho kiliwachukua dakika saba kabla ya mechi kuisha, Real Madrid kupata magoli mawili ya ushindi, yaliofungwa na Ronaldo dakika ya 83 na Marcelo dakika ya 86 na kuifanya mchezo kuisha kwa magoli 3-1

Msimamo wa ma goli ya mechi za jana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2FB Auto Publish Powered By : XYZScripts.com